SIFA NA KUABUDU (PRAISE AND WORSHIP)
MAMBO SABA MUHIMU YA KUYAFAHAMU KUHUSU IBADA NA SIFA
1. SIFA NA IBADA NI MAKAO YA MUNGU – ni mahali akaapo au aketipo Mungu.
• Makao ni kiti, nyumba(hekalu), mji; mahali pa kuishi – patakatifu pake aliye juu (palipoinuka)
• Mungu huketi katika Sifa za Israeli – Zaburi 22:3.
• Hivyo ni lazima uyaheshimu makao ya Mungu
• Usiyanajisi makao ya Mungu
• Usijiinue, usiwe na kiburi, uwe mnyenyekevu mbele za Mungu na wanadamu.
• Sifa ni hekalu la Mungu – ni lazima kusifu kuwe safi na kwa utakatifu.
• Unaposifu ujazo wa Roho Mtakatifu huja; yaani Mungu huja kukaa katika makao yake.
• Uunapomsifu Mungu unaenda kwenye makao ya Mungu moja
kwa moja.

Tokeo la picha la praise and worship
• Shetani alitaka kuyapindua makao ya Mungu mbinguni, na hata makao ya Mungu kupitia sifa! Anataka asifiwe
yeye badala ya Mungu; lakini Mungu ameahidi kuyarejesha mambo yote kuwa mapya!
• Mungu anaheshimu sana sifa na kuabudu, hata amesema sifa zake hatazipa sanamu!
2. SIFA NA IBADA NI MADHABAHU YA KUTOLEA SADAKA MBELE ZA MUNGU ALIYE HAI
• Madhabahu ni meza au mahali pa kutolea sadaka mbele za Mungu – dhabihu ya sifa
• Hivyo: usimchanganye kwa kuishiriki meza ya BWANA YESU na meza ya mashetani (1Kor.10:20-22)
• Usiimbe nyimbo zisizo maana za kiduniani au za kishetani!
• Usilete mitindo ya duniani mbele zake Mungu
• Ukiona madhabahu unapata mvuto wa uwepo wake Mungu na kuabudu – sifa hukuvutia kuabudu.
• Ujitakase na umtakase Mungu uikaribiapo madhabahu ya Mungu- yaani sifa. (Walawi 10:3)
3. SIFA NA IBADA NI SADAKA / DHABIHU YA KUMTOLEA MUNGU
• Usichanganye sehemu ya kuitolea (Zaburi 126:1-2)
• Usilete sadaka / uvumba wa kigeni (manukato) ya kigeni
• Sifa na kuabudu ni manukato / harufu nzuri mbele za Mungu
• Badala ya sisi kutoa wanyama kuwa harufu ya kupendeza mbele za Mungu, sisi tunatakiwa kutoa dhabihu ya
sifa. (Waebrania 13:15)
• Ni dhabihu ya kuitoa miili yetu – ni dhabihu hai iliyo takatifu mbele za Mungu. (Zaburi 40:6)
• Shetani / ibilisi alikuwa ni kwayamasta (Lusiferi = nyota ya asubuhi (kupendeza, kiongozi); nyota = malaika,
Ayubu 38:7) (Ezekieli 28:13;) ambaye alitakiwa kuitumia karama hii kwa ajili ya utukufu wa Mungu; lakini
akaitumia vibaya, badala ya kumtukuza Mungu na kumtolea dhabihu ya sifa Mungu, akajitolea yeye mwenyewe
na akawataka na wengine wote wamsifu yeye badala ya Mungu.
• Leo hii, wengine wanajisahau vivyo hivyo, waimbaji maarufu wamejisahau: badala ya kumtolea Mungu
dhabihu ya sifa na kuabudu, wanajitolea wao wenyewe, wanawataka watu wawatolee wao sifa au wanamtolea
shetani badala ya Mungu anayestahili sifa na utukufu wote!
• Kama kiongozi wa sifa na kuabudu au uimbaji ongoza sifa vizuri, kwani ni hatari kuzitwaa sifa za Mungu na
kumpa mwingine au kujipa sifa wewe mwenyewe.
• Hebu fikiria, unapoimba na kucheza miziki ya disco, dansi, na uimbaji mwingine usio wa kumsifu Mungu,
unamtolea sifa nani? Kama sio wewe mwenyewe, mtu mwingine au shetani?
• Hebu soma kitabu cha nabii (Isaya 42:8).
4. KUSIFU NA KUABUDU NI SILAHA YA VITA VYA KIROHO (Zaburi 149:6-3)
• Iliyotumika kuangusha ngome na kuta za Mji wa Yeriko
• Ilitumiwa na Yehoshafati kuwashinda maadui
• Iliyotumiwa na Paulo na Sila kuwafungua vifungo na kufungua milango ya gereza
• Ni silaha inayoangusha ngome za shetani, wachawi, na kazi za shetani (Fikira, mawazo, na kila kijiinuacho juu
ya elimu ya Mungu)
• Tusiache kuitumia silaha hii na wala tusimuachie shetani aitumie na kutuangamiza sisi badala yake.
• Ni njia ya kumfunga yule mwenye nguvu (shetani, ibilisi na majeshi yake yote) – Zaburi 149:7-8
• Ni silaha ya kuleta uamsho wa kiroho kwa mwamini mwimbaji na kwa kanisa
• Sifa huleta upako na utukufu wa Mungu kwa muimbaji na kwa kanisa, wenye kuziharibu na kuzibomoa kazi za
shetani.
5. KUSIFU NA KUABUDU NI HUDUMA YA KIROHO NA NI CHOMBO CHA HUDUMA YA KIROHO
• Ni chombo cha huduma ya mawasiliano na Mungu
• Kuruhusu utendaji wa karama na huduma za Roho Mtakatifu
• Ni chombo cha kusemezana (kusema zamu kwa zamu, mmoja anazungumza na mwingine anajibu; kuhojiana)
na Mungu
• Ni chombo cha huduma ya neno la Mungu kwa njia ya kuonya, kufundisha, kuelekeza, kuhubiria injili, kuwatia
moyo watu wa Mungu, kukemea na kufariji, na kumbariki Mungu.
• Ni chombo cha kulijenga kanisa la Mungu.
• Ni chombo cha utumishi ambacho kila mtu anatakiwa akitumie ili kumtumikia Mungu – kila mwenye pumzi!
• Ni amri ambayo kila mwenye pumzi anatakiwa akitumie chombo hiki na pia atakitolea hesabu kwa Mungu
(atawajibika) kuhusu matumizi yake.
• Ni chombo cha huduma ya utumishi kwa Mungu, kanisa, na kwa ulimwengu.
• Ni huduma ya utumishi wa milele mbele za Mungu sasa na hata kule mbinguni wanadamu pamoja na malaika
watakatifu wa Mungu.
6. KUSIFU NA KUABUDU NI CHOMBO AU NJIA YA UTAKASO (Mithali 27:20)
• Kusemezana humtakasa mtu – Isaya 1:18; Mathayo 17:1-3
• Unapokuwa mtu wa kupenda kusifu na kuabudu, mawazo mabaya huondoka akilini, hisia, nia na dhamiri
mbaya huondoka; kisha moyo hujaa Neno la Mungu.
• Uimbaji katika Roho na kweli hujenga kiroho; mwimbaji, kanisa, na ulimwengu.
• Ni chombo ambacho humfanya mtu kung’aa na kupendeza mbele za Mungu na hata mbele za wanadamu;
sababu ya kufunikwa na utukufu wa uwepo na upako wa Mungu.
• Kusifu na kuabudu ni pambo zuri la kiroho; Mungu huwapamba wateule wake kupitia sifa na kuabudu (Zaburi 149:1-5)
7. SIFA NA KUABUDU NI CHOMBO AU MFUMO WA KUTENGENEZEA BARAKA ZA MUNGU
• Ni kama mzunguko wa maji kutoka mvuke, kuwa mawingu, kuyeyuka na kuwa mvua kwa joto la jua, maji
kumwagikia ardhini na kuwa sababisho la uotaji wa vyakula vingi na lishe kwa wanadamu na wanyama.
(Amosi 5:8; 9:6; Zaburi 147:7-8)