*BIBLIA INATUFUNDISHA YA KUWA, KUISHI HAPA DUNIANI, KWAKE YEYE AMWAMINIYE BWANA YESU, SI TU KWA BARAKA NA MAFANIKIO YA MWILINI NA ROHONI; BALI PIA NA KUTESWA KWA AJILI YA KRISTO!*

Tokeo la picha la WORD OF GOD
_*Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.*_
(Wafilipi 1:29,30)
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
(Matendo ya Mitume 17:2-4)
Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
Matendo ya Mitume 9:16
Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.
1 Petro 3:17
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
1 Petro 5:10
*JIPE MOYO NA KUJITIA NGUVU, KWA JINA LA YESU, KATIKA HAYO MATESO UNAYOTESWA KWA AJILI YA KUMWAMINI BWANA YESU. AMINA.*