Tokeo la picha la power of prayer

SOMO: Nguvu ya Maombi (The Power of Prayer).
MADA: Jinsi Gani tuombe ili Mungu ajibu maombi yetu?
SEHEMU YA KWANZA.
Tunapaswa Kuomba Juu ya Mambo Gani? Inaendelea......
B. Tunapaswa kuomba kwa ajili ya wengine.
Baada ya kuangalia eneo la kwanza la maombi ya sifa na shukrani kwa Mungu, jambo la pili muhimu kwa muombaji ni kuomba kwa niaba ya wengine.
1 Timotheo2:1-2 inasema
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.

Tokeo la picha la power of prayer
Paulo anasisitiza kabla ya Mambo yote nataka sala, dua,...... Zifanyike kwa aajili ya watu wote.
Hata hivyo wakati mwingine waombaji tunapuuza kuomba kwa ajili ya wengine kwa sababu sisi huwa makini sana na maslahi yetu.
Ni mara ngapi sisi tunaweza kufikiria kuomba kwa ajili ya wengine, hata kama wao hawakuomba maombi yetu?
Nimuhimu kujua kuwa maombi yako kwaajili ya wengine ni Sadaka yenye heshima Kubwa sana mbele za Mungu.
Fikiria kwa makini sana kuwa kuna baadhi ya makundi ya watu ambao tunapaswa kuwaombea, na kama tukifikiri sio muhimu kuwaombea tunaweza jikuta katika hali mbaya kimwili na kiroho pia mfano:
I. Watawala
Kama muombaji ni lazima ujue kuwa utulivu na amani umo mioyoni mwa watawala. Ni muhimu sana kuwaombea watawala ili waweze kufanya mambo yao kwa hekima na Amani ya kutosha. Maandiko yafutayo hutuonyesha umuhimu wa kuombea watawala.
1 Timotheo 2: 1-2. [Ezra 6:10; 1 Nya. 29:18-19] hebu tusome Ezra 6:10 maandiko yanasema.
10 wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima.
ii. Watoto na familia, wenza wetu, ndugu, nk
Waombaji wengi na hasa nazungumzia wakristo tumekuwa na tabia ya kusahau kuombea dugu zetu na watu Wa nyumbani wetu.
Matokeo yake kumekuwa na maumivu mengi kwani shetani anapitia dirisha hilo la watu Wa nyumbani mwetu kutuumiza.
Nimuhimu kuomba hekima, Ulinzi, afya, mahitaji, kazi na maisha yote kwaajili ya Ndugu zetu ili sisi pia tuwe salama katika utumishi wetu.
Tazama kwa makini maandiko haya hapa chini uone ilivyo muhimu kuomba kwaajili ya watu Wa nyumbani mwetu.
1 Nya. 29:19. [Mathayo 19: 13-15; Mwanzo 25: 21,22; 24: 12-14; 18: 23-33; 1 Sam. 1: 10-12; 2 Sam. 12: 15-16; Luke 1:13] ebu tusome luka 1: 13 maandiko yanasema.
13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
Hii inatuonyesha kuwa zakaria alidumu kumuombea Elizabeth mke wake ili apate mtoto.
iii. Kuwaombea walio rudi nyuma na wenye dhambi.
Warumi 10: 1-3. Ni muhimu sana Kumbuka, hata hivyo, kwamba watu hawa lazima kukutana na hali njema za wokovu ili kusamehewa.
Kama kweli shahuku yako ni watu hawa pia waupate ufalme badala ya kuwalaani na kuwakemea ni vizuri kuwaombea ili nao wakumbuke toba na kurejea.
[Matt. 9: 36-38; Luka 23:34; Matendo 7:60]
iv. Wazee, mashemasi, wahubiri, na walimu.
Hili ndio eneo kwa waombaji tunahitaji kuomba sana na kuwaombea watu hawa. Kwamba unamaombi unaombea jambo lolote usiache kuombea roho hizi ni muhimu sana.
Dunia imejaa vitu vya ajabu sana kila mahali ni vilio, wazee wa makanisa wamegeuka wakuabudiwa, walimu wanafundisha wanachojisikia hata kama sio maandiko naomba sana waombaji tuombee sana kundi hili lifanye Mapenzi ya Mungu.
Waefeso 6: 18-20. [ Matendo 4: 25-29; 6: 6; 14:23; 13: 3; 1 The. 5:25; Matt. 9: 36-38; 2 The. 3: 1,2; Ebr. 13:18]
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
19 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena. (Efeso 6:18-20)
Biblia ina mkusanyiko mkubwa wa mifano ambapo watu wa Mungu waliomba kwa niaba ya watu wa Mungu, na kwa sababu hiyo walipata heshima kubwa kwa Mungu na kukomboa watu wengi katika maangamizo.
Hawa ni wachache tu kati ya wengi soma maandiko hayo utajifunza kitu. Nakuomba chukua dakika kadhaa soma:
Musa [Hes. 11: 2; 21: 7; 14: 13-20; Kumb. 9: 18-20,25-29; kutoka. 32: 9-14,31,32].
Samuel [1 Sam. 7: 5-11; 12: 19-25].
Solomon [1 Wafalme 8: 22-54].
Ezra [Ezra 9: 1-15].
Nehemia [Neh. 1: 4-11].
Daniel [Dan. 9: 3-20].
Tujufunze kidogo kwa Yesu - Luka 22: 31,32 (Yesu anamuombe Petro anasema);
31 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Katika Yohana 17: 9-22 (Yesu anawaombe waumini wote anasema).
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
Naamini umeelewa kuwa upo umuhimu Wa kuwaombea wengine katika maombi yako ya kila Siku.
Kumbuka kuwaombe wengine kuonaondoa ubinafsi ndani ya maombi yako na kumfanya Mungu akujibu maombi yako pia kwa haraka sana.